CHAPTER ONE
Kijana wa kiume mwenye umri wa miaka
15 dereva bodaboda akiwa nyumbani kwake
huku akitazama luninga yenye kipindi akipendacho alishtuka baada ya simu yake
kuita.
"nani tena huyu? alijiuliza huku
akienda kuipokea simu
"haloo David unaweza kuja kunichukua
na bodaboda hapa moshi mjini?" aliuliza yule mtu alliye piga simu
"mh!! mbona saizi na pia ratiba yangu
hairuhusu" alisema David huku akitaka kukata simu
"bro kwani shida ni nini wewe si
unataka pesa?" aliuliza yule mpiga simu
"hatakama nina sheria zangu"
alisema David
"David eh!! nisaidie kewapeleka mimi
nimepata mchongo ndo nafanya na huu ni wa pesa ndefu" alisema yule mpiga
simu
"kwani wewe ni nani?" aliuliza
David
"Agh!! ina maana hata sauti yangu
huijui?" aliuliza yule mpiga simu
"hapana sijakufahamu" alisema David
"Ni mimi best yako hapa" alisema
yule mpiga simu
" Ahaa!! kumbe ni wewe kiazi si ungesema
mapema sasa" alisema David
"sasa unaenda au?" aliuliza yule
mpiga simu
"wewe unahisije?" David aliuliza
" mimi nachukulia hilo jibu kama
ndiyo" alisema yule mpiga simu
"sijasema ndio"alisema David
"Acha mambo yako bhana nitakutumia
location ili uende hapo chap sawa eh!!" alisema yule aliyepiga simu kisha
akakata simu
"Dah!! huyu jamaa huyu mpuuzi
kwelikweli amenitoa kwenye tamthilia yangu" David alijisemea huku
akijiandaa ili aende huko alipoagizwa na mda huo ulikuwa ni saa tano usiku.Basi
akatumiwa locationa na kuvaa zake nguo za kazi na kupanda pikipiki/bodaboda
yake kisha akaondoka kuelekea alipoelekezwa.
David alipofika maeneo ya red stone
kama ilivyoonyeshwa kwenye GPS au location aliyotumiwa kisha aliingia ndai ya
klabu hiyo na kusubiri huyo mteja wake kwenye eneo la kuenesha pikipiki, akatoka
baunsa mmoja na kumuuliza
"oya bro unaweza nipeleka ?'' aliuliza
baunsa mmoja
"hapana bro kuna mteja wangu
nnayemsubiri" alisema David
"okay poa ngoja nitembee" alisema
yule baunsa hapohapo akatoka mwanaume mmoja mtanashati na kumfuata David moja
kwa moja yule baunsa alipomwona alishtuka sana na kuamua kumwambia David kwa
kumnong'oneza
"Bro huyo sio mtu mzuri kabisa kama ndo
kaja umchukue jua uko kwenye hatari kubwa vilivile ni muuaji na amekuja na gari
sasa we sepa tu" maneno hayo hakuyatilia maanani na kuamini kilichompeleka
ni kazi si maneno ya watu.Yule mtu alimfuata moja kwa moja wakati huo baynsa
akiongeza spidi ya kutembea ili aondoke
"Habari yako David?" alisalimu yule
mtu
" salama sijui wewe?" alijibu David
huku akijawa na wasiwasi mno na
kujiuliza moyoni imekuwaje amenifahamu jina ila aliamua kukaushia
"naomba nipeleke uwanja wa ndege"
alisema yule mtu
"nini uwanja wa ndege?" aliuliza
kwa hasmaki
" usijali uko na mimi alafu
nilijisahau naitwa Jacob Stewart" alisema yule mtu kwa
kujitambulisha(Jacob)
"ahaa! sawa mr Jacob hakuna njia
mbadala?"aliuliza David
"mimi naishi karibu na kanisa la
K.K.K.T" alisema Jacob
"sawa labda tupitie hii ya lami"
alisema David
"mh!! mimi dsiijui hiyo njia maana mimi
ni mgeni ila wewe twende ilimradi tufike kunapokusudiwa au unasemaje?"
aliuliza Jacob
"haya sawa ila ni sh 5000"alisema
David
"wewe usijali rwende" alisema Jacob
kisha akapanda bodaboda na kuanza safari walipofika kwenye njia panda ya
kuelekea mawazo Jacob aliomba ashuke ili ajisaidie ile amesimamisha bodaboda tu
alishtukia amepigwa na kitu kizito kichwani na pia shinhoni alihisi kitu chenye
ncha kali kimemchaa na maji ya moto yanaanza kumtoka hapo alimuona Jacob na
kisu chake kinachodondosha matone ya damu. Jacob alimuangalia akiwa anatapatapa
kutafuta hewa huku mikono yake ikiwa shingoni kuzuia damu.Jacob alimtemea mate
na kuichukua bodaboda ya David na kuondoka zake huku akimuacha David hali mbaya
sana na damu nyingi zinamtoka.
Comments
Post a Comment