CHAPTER TWO.
Miaka kumi
baada ya tukio.
Kijana mmoja
anashuka kwenye ndege kwenye uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere huku akivaa
nguo nzuri za gharama na kupokelewa na mwanaume mwingine aliyekuwa anamsubiri.
"habari yako bosi pole kwa safari"
alisema yule mtu aliyekuwa anamsubiria
"salama James za siku nyingi?"
aliuliza yule bosi kwa sauti yake ya kukwaruzakwaruza kama mtu aliyekabwa hali
hiyo ilimuuma ila hakuwa na jinsi na ameshaanza kuzoea
"salama mkuu" alisema James
"Twende zetu home tutajua la
kufanya"alisema bossi
"sawa bosi"alisema huku akitaka
kuchukua mizigo ila alikuta bossi kashaichukua na kuiweka kwenye buti ya gari
"sasa bosi si uache nikusaidie"
alisema James
"unisaidie..... KWANI UMESIKIA MIMI NI
MLEMAVU?" aliuliza bossi kwa jazba
"hapana mkuu"alijibu Jamesi kwa
hofu
"Dah!! saamahani bhana alisema bossi
huku akiachia ule mzigo aliokuwa nao ili James aubebe, hali hiyo ilamshangaza
sana James maana alikuwa anajua kuwa mkuu wake ni mkorofi pia alihisi ni mtu
mwenye hasira muda wote ila alichoambiwa na ukweli wenyewe ni vitu viwili
tofauti.Wakapanda gari na kuanza safari ya kwenda Kilimanjaro.
Mjini Moshi kwenye jengo la kilimani
ofisi za kampuni kubwa ndani ya ofisi kuna mwanaume mwenye umri wa miaka 30
akiwa ameweka miguu juu ya meza na mbele ya meza kuna utambulisho wa jina lake
ambalo ni David ambaye ni mtoto wa bwana Jacson Urasa ambaye alifariki na
kumuachia hizo mali ambazo zilisimamiwa na mama wa kambo aliyeitwa mama James.
" habari yako mwanangu"
ilisikika sauti ya mwanamke ikimsalimia David naye alikuwa ni mama James
"salama shkamoo mama" alijibu
David
"marhabaa umeshndaje?"
aliuliza mama James
" salama sijui wewe mama?"
aliuliza David
"mimi niko salama nimepata habari
kutoka kwa James kwamba yule mgeni anakuja sasa tujiandae" alisema mama
James
"sawa mama anakuja saa ngapi?"
David aliuliza
"atafika jion nahisi atakuwa
hotelini labda kindoroko ila sijajua hivyo fanya ukampokee sawa?" alisema
mama James
"sawa mama kwani si tuende
wote?" aliuliza David
"mh!! ila nina kazi nyingi
sana" alisema Mama James
"mh! mama kazi haziishagi twende
wote" alisema David
"tangu uache bodaboda umekuwa
mstaarabu sana" alisema mama James "okay sawa tutaenda wote na
usiendeshe gari kama kichaa" aliongezea
Upande
wa bossi na James walikuwa safarini kuelekaea Kilimanjaro huku James akiwa na
furaha sana ila Bossi wake akiwa na wasiwasi.
"Bossi mbona unawasiwasi?"
aliuliza James
"nawaza James alafu usiniite
Bossi" alisema Bossi
"sasa unataka nikuiteje nikuite
jina lako ili kilamtu akujue au nikuite hivihivi?" aliuliza James
"Haya bhana ila twende kufuata
mpango wetu au unasemaje? aliuliza Bossi
"ndoivo tunavyotakiwa"alijibu
James huku akitabasamu
"ila bosi nilitakiwa nikuite wewe"
alisema Bossi
"acha ujinga wewe unastahili hili
jina kwahiyo sitaki kuusikia huvyo na wewe unajua kwanini unaitwa
hivyo"alisema James
"kwani nimekataa?" alisema Bossi
nayo safari ikayoyoma walipokaribia moshi walipiga simu nyumbani ili kuwapa
taarifa ya safari yao
"Halo shkamoo mama" alisema
James kumsalimia mamaye
"marhaba mwanangu hujambo?"
aliuliza mama James
" sijambo sisi ndo tumefika
kiborloni" alisema James
"Sawa" alisema James kisha
akakata simu
"Haya tutawakuta kwanye kituo cha
mabasi cha moshi mjini" alisema James kumwelekea Bossi wake
" ok sawa" bossi alijibu huku
akipiga muayo
Huku
nyumbani kwa mama Jamesi akiwa anajiandaa akampigia simu David ajiandae
kumpokea huyo mgeni atakayekuja ambaye hata wao hawamjui kwa sura na ni mgeni
muhimu katika kampuni ambapo wanamsubiria ili kuisaidia kampuni dhidi ya
kufilisika.Baada ya David kufika tu walipanda gari na kuanza safari yao
kuelekea kituo cha mabasi Moshi mjini walipofika walishuka na kumsubiri mgeni
wao kwenye kiamgahawa ka fresh coach. Mji ulikuwa na baridi kiasi ambayo
ilifanya mji kupoa na pia kelele za watu kama nyuki kwenye mzinga zilifanya mji
uendelee kupendeza ila hali ilibadilika baada ya James kufika na mgeni wake
papo hapo hali joto iliongezeka na dunia yote ikakaa kimya kanakwamba walipata
uziwi wa ghafla nao muda ulisimama ukawa unawnda taratibu sana hawakuamini
kilichoendelea.
"ha...ha...haiwezekani" alisema
David
" nini eh!! mbona un...." mama
James hakuweza kumalizia baada ya kumwona Bossi hali yake ikabailika na kuanza
kutapatapa kama samaki nje ya maji asijue la kuongea huku akimhisi David kuwa
amepanga njama za kumuharibia na kumpindua ila haikuwa hivyo maana hata yeye
alikuwa na hofu ya kutosha
Comments
Post a Comment